. :
Home » » CCM NA CHADEMA WAGOMBANIA MTI WA BENDERA

CCM NA CHADEMA WAGOMBANIA MTI WA BENDERA

Written By KITUMBO GALAXY on Monday, February 4, 2013 | 6:37 PM




SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.

Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma

Vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.

Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.

“Baada ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa nguvu, jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,”alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Baadhi ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime), Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti Maalumu).

Baadhi ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa Chadema na kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa ikipepea eneo la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).

“Kwanza wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM kuruhusiwa kufanya maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi kukataza mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.

“Kwa nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu wanafanya? Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama katika kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na tukaheshimu mamlaka,” alisema katibu huyo.

Pia tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.

Mambo alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za majeruhi hao.

Chanzo: Gazeti la Mwanachi
 ZIFUATAZO NI PICHA ZIKIONESHA UGOMVI HUO
 

Smiley faceSmiley faceSmiley faceSmiley faceSmiley face

Share this post :

+ comments + 1 comments

October 17, 2013 at 1:42 PM

keep it up kitumbo

Post a Comment

 
Support : Kitumbo | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KITUMBO GALAXY - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger