. :

WANAOTEMBELEA

KALI ZA WIKI HII

SAMATTA: GOLI LANGU DHIDI YA CAMEROON NI OMBI LANGU LA MSAMAHA KWA WASHABIKI NA NAAMINI WAMENISAMEHE

MBWANA Samatta amesema kuwa anaamini goli la ushindi alilofunga dhidi ya Cameroon linatosha kumsafisha kwa mashabiki wake.
 

Hiyo imekuja baada ya mashabiki wa soka kuwazomea pamoja na Thomas Ulimwengu wakati Stars ikicheza na Zambia, mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.
 

Nikutokana na kuchelewa kuripoti kambini kujiwinda na mchezo huo wa kirafiki na Chipolopolo mwakajana.
 

Kitendo hicho kilimkasirisha kocha Kim Poulsen ambaye aligoma kuwapanga kwenye kikosi ambacho kilicheza mtanange huo.
 

Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao hilo pekee, likizamishwa na Mrisho Ngassa kwa shuti la mwendo mrefu.
 

"Naamini ushindi huu utakuwa umewafurahisha mashabiki na kurudisha imani kwetu." alisema Samatta.
 

Alisema haikuwa lengo leo kuchelewa kujiunga na kambi ya timu isipokuwa ni mambo tu yaliingiliana.
Ahsante sana shafii dauda

HUYU NDIO MTOTO WA DARASA LA SITA ALIYEFUMANIWA AKIWA NA DEREVA BODABODA

http://api.ning.com/files/Y7XrEGzfaFfHd8wYjo*MnVoljeNXI4K4akiu9hd9qDvKI1a*snHGgLuYpCjNepnAYh6iKZOJgmxAYGAS0KhGXyJe0Ga2EnRB/DENTI.jpgDenti aliyefumaniwa (nyuma ya wa kwanza kushoto) akipelekwa shuleni na ndugu zake baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo chanzo makini kimeeleza kuwa mtego wa kunaswa kwa denti huyo anayesoma darasa la sita, uliandaliwa na dada zake wanaomlea kufuatia wazazi wao kufariki dunia.
Baada ya paparazi wetu kujiridhisha na picha za tukio hilo, aliwafuata dada zake pamoja na walimu wa shule hiyo lakini walikataa kutoa ushirikiano.
“Utuhoji ili iweje? Swala hili tumelipeleka pale shule na tutalimaliza shuleni kwani hawa wote ni vijana wetu, hatuhitaji habari hizi zitoke kwenye vyombo vya habari,” alisema kwa ukali dada mmoja wa mwanafunzi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Alipotafutwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na kuulizwa juu ya tukio hilo, alikataa kuzungumzia chochote akidai shule yake haihusiki na tukio hilo kwa kuwa lilitokea nje ya maeneo ya shule.
“Sioni sababu ya kutaja jina langu, mimi ni mwalimu mkuu wa shule hii, fumanizi  hilo halituhusu kwa sababu halikutokea kwenye madarasa wala vyoo vya shule yetu,” alisema mwalimu huyo.

PICHA 15 ZIKIONYESHA MELI YA MV VICTORIA AKIWAKA MOTO, NA HARAKATI ZA KUUZIMA MOTO HUO

MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.

Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.

Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.

Hii ndiyo sehemu iliyokuwa na mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea ndipo cheche za moto zikapenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuzua motomkubwa.
Juhudi zikiendelea kwa maafisa wa kikosi hicho kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.

Hata hivyo moto huo uliodumu kwa saa kadhaa ulifanikiwa kuzimwa ndipo juhudi za kuyatoa magodoro na mito yote ya makochi yaliyokuwemo ndani ya hifadhi ya mizigo ili kuhakiki uharibifu pamoja na kufanya tathimini kwa mali zilizo haribika.
Kwa umakini zaidi kuhakiki moto huo.
Wafanyakazi wa MSC wakitumia mashine maalumu ya kushushia mizigo ya kampuni hiyo wakitoa mabaki ya vitu vilivyounguzwa na moto.
Mtoto huo kama ungefanikiwa kuiteketeza meli ya Mv Victoria ingekuwa hasara kubwa sana kwa shirika la Marine Service kukosa chombo cha usafiri majini bandari za miji ya Mwanza, Kemondo na Bukoba, kwani  meli hii ndiyo meli pekee iliyosalia kwa safari hizo.

Ikumnbukwe kuwa Mv. Serengeti kwa sasa haiko shughulini na Mv. Bukoba ndiyo hivyo tena ilizama mwaka 1996 na mamia ya ndugu zetu.

Juhudi za ushushaji mizigo iliyoungua zikiendelea.


Ndani ya masaa mawili moto huo ulikuwa umedhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji waliowasili katika eneo hilo muda mchache baada ya moto kuanza wakitumia gari lenye namba za ausajili STK 1965 Mali ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Mmliki wa magodoro pamoja na mito ya makocho iliyoteketea kwa moto aliyejitambulisha kwa jina moja la Ogunya amesema kuwa amepoteza magodoro 180 pamoja na mito 80 katika tukio hilo.


Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa majini na nchi kavu(SUMATRA) kanda ya ziwa Josephat Loisimaye amesema kuwa uzembe wa viongozi wa MSC ndio ambao ulisababisha kutokea kwa moto huo.
Amesema kuwa viongozi wa MSC walipashwa kuchukua tahadhari mapema kabla ya kuanza uchomeleaji katika sehemu ya Meli hiyo na kueleza kuwa wanasubiri ripoti ili waweze kuchukua hatua zaidi.
Hata hivyo Loismaye amesema kuwa Meli ya Mv Victoia iko salama na itaendelea na safari zake kwenda Bukoba leo usiku kwa kuwa moto huo haukuweza kuathiri mfumo wa injini ya Meli na kukipongeza kikosi cha zimamoto kutokana na kufika mapema na kuzima moto huo vinginevyo Meli hiyo ingeliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.

MASKINI! MTOTO MCHANGA ATUPWA DAMPO LA TAKATAKA


ZIKIWA zimepita  siku takriban tano toka kukutwa kwa mwili  wa mtoto mchanga katika eneo la Semtema jirani na makazi ya  wanafunzi wa chuo kimoja cha dini mkoani Iringa, simanzi na majonzi zimeendelea kutanda katika Manispaa hiyo baada ya mtoto mwingine wa jinsi ya kike kutupwa katika dampo la taka eneo la Stendi ya M.R mjini Iringa.

Wakizungumzia  matukio hayo ya wanawake wasiofahamika  kufanya vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto wanaowazaa, baadhi ya akina mama wamelitaka jeshi la polisi na jamii nzima kusaidiana kuendesha misako dhidi ya  wanawake  wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili.


Sarah Sanga, mkazi wa Miyomboni mjini hapa alisema kuwa  matukio ya wanawake kutoa mimba na kutupa watoto  yameendelea na kuwa ni tishio katika Manispaa ya Iringa.


Bwana Said alishauri wanawake kuwafichua wenzao ambao siku za karibuni walionekana na mimba na ghafla mimba hizo kutoweka kwani  wanaweza kuwa wahusika lakini akawalaumu wanaume kwamba wanaweza kuwa chanzo cha tatizo hilo.


Mkuu  wa Wilaya  ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizungumzia tukio hilo amewataka mabinti na vijana wilayani hapo kuepuka  kupeana  mimba bila kuwa na uhakika wa ndoa.


“Serikali ya wilaya itaendelea kutoa elimu zaidi kwa vijana ili  kupunguza tatizo la watoto  kutupwa katika wilaya ya Iringa,”
alisema 


Jeshi la  Polisi Mkoa wa Iringa, limethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuahidi  kuendelea na msako mkali  ili kuwakamata  wahusika.

Rage kufikishwa kortini


Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage na wenzake wakipambana na kada wa Chadema             Dodoma
MBUNGE wa Tabora Mjini Ismal Aden Rage anatarajia kufikshwa mahakamani wakati wowote kutoka na tuhuma za kushiriki na kumpiga kada wa Chadema  wakati wa vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa Chadema na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Rage wakati walipokuwa wakigombea mlingoti wa bendera, kitendo kilichosababisha watu watatu kujeruhiwa katika tukio hilo wikiendi iliyopita mjini Dodoma.
Akizungumza na Habarimpya.com mjini Dodoma Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kuwa wanaandaa utaratibu wa kumfikisha Mbunge huyo Kortini baada ya jalada la kuhusika katika vurugu hizo na kumpiga kada huyo wa Chadema kukamilika.
Kamanda Misime amesema kuwa baada ya jalada hilo kukamilika litafikishwa kwa  Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), "Ni kweli tumepokea malalamiko ya Chadema na tunaandaa jalada ili kuwasilisha kwa mwanasheria wa Serikali,” alisema Misime.
Kwa upande wake Rage alikanusha kuhusika katika tukio la kumpiga kada huyo na kusema“Sikumpiga. Historia yangu inaonyesha kuwa sijawahi kushiriki vitendo vya vurugu wala mapigano kwa sababu yoyote ile. Mimi siyo mhuni wa kupiga mtu. Nilichofanya ni kumlinda yule kijana asipigwe na wanaCCM waliojaa hasira kwa yeye kuingilia mkutano wetu,” alisema Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.

VITAMBULISHO VYA TAIFA SASA KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZ UJAO

RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehaidi kuwasaidia Mamlaka ya   Vitambulisho (NIDA)  kwa kuiwezesha  kupata fedha  kwa ajili  Vitambulisho vya Taifa  ili  kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watu wote watakuwa na vitambulisho vya Taifa vitakavyo tumika katika uchaguzi huo.

Aidha  Rais  Kikwete  aliitaka NIDA  kutoa vitambulisho kwa watu wanaotakiwa na kuchukulia hatua za kisheria wale  watakaokiuka sheria ya usajili wa vitambulisho hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa  leo na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo  uliofanyika  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa  kutoa taarifa zao kwa uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha  zoezi hilo.
Aliwataka viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.
Naye Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Dk. Emmanuel  Nchimbi alisema ni  muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya kitaifa.
Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI, Mifumo ya mawasiliano yasimu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.
Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni  vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini  takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha  mpango huo kwa muda utaotakiwa.
Chanzo: mrokim.blogspot.com

RIDHIWANI KIKWETE AIKANA TANZANIA LOAN SOCIETY.....ADAI YEYE SI TAPELIHabari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .

Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe. lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata twitts juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack Obama kuja tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.

kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa mliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na zoezi hili.
 
 Lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao juu ya hili

MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
AKHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.

"SINA UGOMVI WOWOTE NA FREEMAN MBOWE"...ZITTO KABWE.
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amesema hakuna mgogoro kwenye chama chake kama inavyoelezwa isipokua kuna watu wachache ambao wanataka kugombanisha viongozi wa CHADEMA.


Hii ni kauli ambayo Zitto aliitoa kwenye mkutano na wananchi Kigoma ambapo alisema kwamba CHADEMA ni wamoja isipokua ni watu wachache ndio wamekua wakieneza chokochoko.


Namkariri akisema “nataka mkae mnajua hakuna mgogoro wala tofauti ya mawazo, yani hakuna kitu ambacho mimi nasema twende hivi Mbowe anasema twende hivi isipokua kuna watu wanasema kwamba Zitto, Mbowe anakuchukia au Mbowe, Zitto anataka kukupindua....

Wanasema hivyo lakini mimi nataka kuwaambia watu wa Kigoma kwamba hakuna tatizo na pangekua na tatizo lolote ningeshawaambia, kuna watu wanapandikiza mbegu za chuki, kuna watu wanajaribu kufarakanisha viongozi na kujaribu kuonyesha kwamba kuna tofauti”


Zitto aliongeza kwamba: “sisi tutakua ni wajinga sana kukubali kugombanishwa, hatuwezi kukubali kuingia kwenye mgogoro kama ambao NCCR MAGEUZI waliingia kwa sababu leo CHADEMA ikianguka, ikapasuka hapatatokea chama chochote kingine cha upinzani chenye nguvu kwa miaka mingine 20 na watakaoumia ni nyie wananchi, sababu panapokua na upinzani imara wanaofaidika ni nyie, mawazo tofauti ndani ya bunge yanasikika kupitia vyama vya upinzani, mpinzani wako ni lazima atengeneze mbegu za chuki ili mgombane mfarakane”

TAMKO LA DIAMOND KUHUSU MGANGA WAKE


Naweza kusema kwamba mwaka huu kwa Diamond utakuwa kama ni wa msala juzi juz tulisikia kwamba aliletewa fujo katika show yake iliyofanyika ndani ya Maisha Club.
Leo asubuhi baada ya magazeti ya siku kutoa vinjwa vingi vya habari vilikuwa vikisema kwamba Mganga wa Diamond amejitokeza na anatokea maeneo ya Magomeni "Ustadhi Yahya Michael"sisi kama team nzima ya Fetty The Best baada ya kusikilia habari kama hizi tuliamua kumpigia simu Diamond na akasema kwamba hamfahamu huyo mganga na wala hajiweki katika mambo ya kishirikina ni uongo mtupu"alisema Diamond.
Hili ndiyo gazeti ambalo limechukua nafasi kubwa ya story kati ya diamond na mganga wake 

  Picha ni Bw.Yahya Michael ambaye alijitokeza na kuweka wazi kwamba yeye ndiye Mganga wa Diamond Platinum....

CCM NA CHADEMA WAGOMBANIA MTI WA BENDERA
SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.

Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma

Vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.

Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.

“Baada ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa nguvu, jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,”alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Baadhi ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime), Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti Maalumu).

Baadhi ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa Chadema na kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa ikipepea eneo la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).

“Kwanza wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM kuruhusiwa kufanya maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi kukataza mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.

“Kwa nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu wanafanya? Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama katika kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na tukaheshimu mamlaka,” alisema katibu huyo.

Pia tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.

Mambo alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za majeruhi hao.

Chanzo: Gazeti la Mwanachi
 ZIFUATAZO NI PICHA ZIKIONESHA UGOMVI HUO
 

Smiley faceSmiley faceSmiley faceSmiley faceSmiley face

 
Support : Kitumbo | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KITUMBO GALAXY - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger