. :
Home » » RIDHIWANI KIKWETE AIKANA TANZANIA LOAN SOCIETY.....ADAI YEYE SI TAPELI

RIDHIWANI KIKWETE AIKANA TANZANIA LOAN SOCIETY.....ADAI YEYE SI TAPELI

Written By KITUMBO GALAXY on Thursday, February 7, 2013 | 1:28 AM



Habari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .

Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe. lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata twitts juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack Obama kuja tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.

kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa mliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na zoezi hili.
 
 Lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao juu ya hili

MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
AKHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.

Share this post :

Post a Comment

 
Support : Kitumbo | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KITUMBO GALAXY - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger