. :
Home » » "SINA UGOMVI WOWOTE NA FREEMAN MBOWE"...ZITTO KABWE

"SINA UGOMVI WOWOTE NA FREEMAN MBOWE"...ZITTO KABWE

Written By KITUMBO GALAXY on Monday, February 4, 2013 | 6:40 PM



.
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amesema hakuna mgogoro kwenye chama chake kama inavyoelezwa isipokua kuna watu wachache ambao wanataka kugombanisha viongozi wa CHADEMA.


Hii ni kauli ambayo Zitto aliitoa kwenye mkutano na wananchi Kigoma ambapo alisema kwamba CHADEMA ni wamoja isipokua ni watu wachache ndio wamekua wakieneza chokochoko.


Namkariri akisema “nataka mkae mnajua hakuna mgogoro wala tofauti ya mawazo, yani hakuna kitu ambacho mimi nasema twende hivi Mbowe anasema twende hivi isipokua kuna watu wanasema kwamba Zitto, Mbowe anakuchukia au Mbowe, Zitto anataka kukupindua....

Wanasema hivyo lakini mimi nataka kuwaambia watu wa Kigoma kwamba hakuna tatizo na pangekua na tatizo lolote ningeshawaambia, kuna watu wanapandikiza mbegu za chuki, kuna watu wanajaribu kufarakanisha viongozi na kujaribu kuonyesha kwamba kuna tofauti”


Zitto aliongeza kwamba: “sisi tutakua ni wajinga sana kukubali kugombanishwa, hatuwezi kukubali kuingia kwenye mgogoro kama ambao NCCR MAGEUZI waliingia kwa sababu leo CHADEMA ikianguka, ikapasuka hapatatokea chama chochote kingine cha upinzani chenye nguvu kwa miaka mingine 20 na watakaoumia ni nyie wananchi, sababu panapokua na upinzani imara wanaofaidika ni nyie, mawazo tofauti ndani ya bunge yanasikika kupitia vyama vya upinzani, mpinzani wako ni lazima atengeneze mbegu za chuki ili mgombane mfarakane”

Share this post :

Post a Comment

 
Support : Kitumbo | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KITUMBO GALAXY - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger